Nyimbo Za Kristo | Song Logic

NZK 190 – Raha Yangu Yote, Bwana

190. Raha Yangu Yote, Bwana

Forever Here My Rest Shall Be

Key: A♭ Major

1

Raha yangu yote, Bwana, I mbavuni pako;
Mimi sina haja tena ila kifo chako.

2

Mwokozi uliyekufa, nawe ndiwe Mungu,
Kifo chako ni kwa dhambi, ziondoe zangu.

3

Nioshe na niwe wako, nawe uwe wangu;
Nioshe damuni mwako liwe fungu langu.

4

Nioshe si miguu tu, osha tangu nyayo,
Hata kichwa changu juu, na ndani ya moyo,

5

Na iwe kafara damu nifanyapo kazi,
Hata imani itimu, nikwone,Mwokozi.