Nyimbo Za Kristo | Song Logic

NZK 170 – Jina Langu Limeandikwa Je

170. Jina Langu Limeandikwa Je

Lord, I Care Not for Riches

Key: A♭ Major

1

Sitafuti mali, wala utajiri;
Nataka kwa yakini nipate Mwokozi.
Chuoni mwa Ufalme, niambie Yesu,
Jina langu yakini limeandikwa, je?

Limeandikwa, je? Jina langu huko?
Kitabuni mbinguni, limeandikwa, je?

2

Dhambi zangu ni nyingi, ni kama mchanga,
Lakini damu yako, Mwokozi, yatosha;
Kwani umeahidi: zijapo nyekundu
Zitakuwa nyeupe ilivyo theluji.

Limeandikwa, je? Jina langu huko?
Kitabuni mbinguni, limeandikwa, je?

3

Mji mzuri sana, wa majumba makuu,
Walipo malaika, mji bila ovu;
Wakaapo walio na mavazi safi,
Limeandikwa sasa, jina langu huko?

Limeandikwa, je? Jina langu huko?
Kitabuni mbinguni, limeandikwa, je?