Nyimbo Za Kristo | Song Logic

NZK 107 – Nipo Bwana, Nitume

107. Nipo Bwana, Nitume

Hark! The Voice of Jesus (SDAH 359)

Key: D♭ Major

1

Sauti ni yake Bwana, "Kwenda nani tayari?"
Mavuno yanakawia, Nani atayavuna?
Kwa kudumu anaita, Zawadi atatoa;
Nani atakayejibu, "Nipo Bwana nitume."

2

Kama huwezi safari, Hata nchi za mbali,
Pana watu karibuni, Wasiomjua Yesu;
Kama huwezi kusema, Jinsi ya malaika,
Waweza kuutangaza, Upendo wa Mwokozi.

3

Ingawa huwezi kuwa, Mkesha mlangoni,
Ukiwatolea watu, Nafasi ya uzima;
Kwa sala na kwa sadaka, Watoa msaada,
Kama Harun mwaminifu, Kuinua mikono.

4

Roho za watu zikifa, Bwana akikuita,
Usiseme kwa uvivu, "Hakuna kazi kwangu".
Kwa furaha anza kazi, Ile aliyokupa,
Ukajibu mara moja, "Nipo Bwana nitume".