101. Yesu Akwita
Jesus is Tenderly Calling Today
Key: C Major
1
Yesu Akwita, Akwita wewe,
Uje leo, uje leo,
Kwani kusita, akwita wewe,
Unatanga upeo.
Msikie, msikie,
Yesu akwita,
ujitoe moyo sasa.
2
Waliochoka, na wapumzike,
Uje leo, uje leo,
Wenye mizigo, wenye huzuni,
Wapate mapumziko.
Msikie, msikie,
Yesu akwita,
ujitoe moyo sasa.
3
Anakungoja uliye yote,
Uje leo, uje leo,
Uliyekosa, usijifiche:
Woshwe, uvikwe nguo.
Msikie, msikie,
Yesu akwita,
ujitoe moyo sasa.
4
Yesu asihi wakawiao,
Waje leo, waje leo,
Watafurahi waaminio;
Amka, upesi, Njoo.
Msikie, msikie,
Yesu akwita,
ujitoe moyo sasa.