Nyimbo Za Kristo | Song Logic

NZK 091 – Kaa Nami

91. Kaa Nami

Abide with Me (SDAH 50)

Key: E♭ Major

1

Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani, Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu kaa nami.

2

Siku zetu hazikawi kwisha;
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi;
Usiye na mwisho, kaa nami.

3

Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe Bwana, kaa nami.

4

Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako kaa nami.

5

Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi;
Siku zangu zote kaa nami.