29. Yesu, Nakupenda
My Jesus, I Love Thee (SDAH 321)
Key: F Major
1
Yesu nakupenda, u mali yangu, Anasa za dhambi sitaki kwangu:
Na mwokozi aliyeniokoa Sasa nakupenda, kuzidi pia.
2
Moyo umejaa mapenzi tele Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea Sasa nakupenda, kuzidi pia.
3
Ulipoangikwa msalabani Tusamehewe tulio dhambini;
Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia.
4
Mawanda mazuri na masikani Niyatazamapo huko mbinguni,
`Tasema na taji nitakayovaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia.