Nyimbo Za Kristo | Song Logic

NZK 004 – Jina La Yesu Salamu

4. Jina La Yesu Salamu

All Hail the Power of Jesus

Key: G Major

1

Jina la Yesu, salamu! Lisujidieni,
Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni
Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni

2

Enzi na apewe kwenu, watetea dini;
Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni
Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni

3

Enyi mbegu ya rehema nanyi msifu;
Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni
Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni

4

Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani
Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni
Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.

5

Kila mtu duniani msujudieni
Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni
Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.

6

Sisi na wao pamoja tu mumo sifani.
Milele sifa ni moja, na mpeni
Milele sifa ni moja, na enzi mpeni