Nyimbo Za Kristo | Song Logic

NZK 001 – Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu

1. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu

Holy, Holy, Holy (SDAH 73) (SDAH 073)

Key: D Major

1

U Mtakatifu! Mungu mwenyezi!
Alfajiri sifa zako tutaimba;
U Mtakatifu , Bwana wa huruma,
Mungu wa vyote hata milele.

2

U Mtakatifu! Na malaika
Wengi sana wanakuabudu wote;
Elfu na maelfu wanakusujudu
Wa zamani na hata milele.

3

U Mtakatifu! Ingawa giza
Lakuficha fahari tusiione,
U Mtakatifu! Wewe peke yako,
Kamili kwa uwezo na pendo.